Startimes

Startimes

Azam Tv.

Azam Tv.

Tabibu Tv

Tabibu Tv

Kurasa Zangu

Wednesday, October 19, 2016

Fahamu kuhusu maajabu ya mti wa mvunge katika tiba.

Mti wa mvunge au Miegeya au Kigelia Africana kama unavyojulikana katika sayansi ya mimea ni mti unaostawi katika maeneo yenye ardhi yenye unyevunyevu na una tabia ya ustawi kama mwembe na huzaa matunda yanayofanana na mbuyu.Mti huo unaojulikana kwa jina la sausage tree katika lugha ya kiingereza hukua na kufikia urefu wa mita 20, hupatikana katika nchi nyingi za Afrika na baadhi ya nchi za bara la Asia. 

Mti huo unaoelezwa kuwa na uwezo wa kuongeza maumbile ya kiume na kwa upande wa wanawake una uwezo wa kuongeza makalio, mahips na matiti.
Sambamba na hayo, mti huo unaostawi zaidi katika mikoa ya Tanga, Pwani, Mbeya, morogoro na mingine, unaelezwa kuwa na uwezo wa kukabiliana na ugonjwa wa saratani ya kizazi na ngozi, malaria na nimonia. Faida zingine za mazao ya mti huo ni kutibu vidonda, matatizo ya tumbo kwa watoto, maambukizi ya fangasi na bakteria.

Hutibu upungufu wa nguvu za kiume, ugumba kwa wanaume na kuongeza hamu ya tendo
Utafiti uliofanywa na watafiti Owolabi na Omogbai mwaka 2007, ulibaini kuwa matunda, mizizi na majani ya mvunge yana uwezo wa kutibu tatizo la ugumba kwa wanaume, kukosa hamu ya tendo la ndoa pamoja na upungufu wa nguvu za kiume.
Mtafiti mwingine anayefahamika kwa jina la Dada, katika utafiti wake mwaka 2010, alioufanya maabara kwa kutumia samaki aina ya kambale alibaini kuwa, unga unaotokana na matunda ya mvunge yaliokaushwa huongeza uwezo wa kuzaliana kwa samaki hao.Kwa mujibu wa mtafiti huyo, uwezo huo hutokana na misombo (compounds) ya biflavonoid na xanthone vinavyopatikana katika mazao ya mti huo.Mtafiti mwingine anayejulikana kwa jina la Azu katika tafiti zake alizozifanya mwaka 2005, 2009 na 2010 aligundua kuwa, matunda ya mvunge yana uwezo wa kuongeza kiwango cha mbegu za kiume na kuongeza ubora wake kwa asilimia 70 zaidi.

Pia matunda hayo yana uwezo wa kuongeza hamu ya tendo, kuweka sawa kiwango cha homoni za uzazi, hivyo kuongeza uwezo wa kutungisha mimba.Tafiti zingine zilizofanywa na watafiti Yukubu mwaka 2007 na Monga mwaka 1999, ulibaini kuwa mazao ya mti huo huongeza nguvu za kiume. Kwa upande wake mtafiti Jeong katika utafiti wake aliofanya mwaka 1999, alibainisha kuwa mazao ya mvunge yana utajiri mkubwa wa misombo (compounds) ya bioflavonoids, saponins na tannins.

Ifahamike kuwa misombo hiyo huitajika mwilini katika kuboresha afya ya mfumo wa uzazi hasa wa mwanaume Pamoja na hayo inaelezwa kuwa, matunda ya mvunge yana sumu hivyo inapendekezwa kutumika kiasi kidogomno kiasi cha 100 mg/kg, kwani matumizi ya kiasi kikubwa huweza kuleta madhara. Aidha, tafiti zinaeleza kuwa, unaweza kutumia majani au magome ya mti huo kupata faida hizo badala ya kutumia matunda.

Jinsi ya kutumia kupata faida hizo
Kupata faida hizo kwa kutumia magome ya mti huo, chukua magome na uyakaushe kivulini (sio juani), baada ya kukauka, saga magome hayo ili upate unga.
Chota unga huo kiasi cha gramu 700 (karibu na robo tatu kilo), changanya na maji kiasi cha lita kiasi cha lita 6. Mwenye tatizo anatakiwa kunywa mchanganyiko huo kwa kiasi cha robo lita kila siku.

Hutibu maambukizi ya bakteria na fangasi
Utafiti uliofanywa na Chuo Kikuu cha Natal, kilichopo Durban, Afrika Kusini, ulibaini kuwa, magome ya mti huo yana uwezo mkubwa wa kupambana na bakteria mbalimbali wakiwemo Escherichia coli, Pseudomonas aeruginosa, Staphylococcus aureus.Pia magome hayo yana uwezo mkubwa wa kupamba na fangasi wa aina mbalimbali wakiwemo Candida albicans. Ifahamike bakteri na fangasi hao, husababisha maambukizi katika njia ya mkojo ama U.T.I (Urinary Tract Infectio) kwa lugha ya kiingereza.

Aidha, fangasi aina ya candida albicans ni miongoni mwa fangasi wanaowasumbua wanawake hasa pale wanapokuwa kwa wingi katika sehemu zao za siri. Matokeo ya utafiti huo yanafanana na matokeo ya utafiti uliofanywa na watafiti kutoka Chuo Kikuu cha Nigeria wakishirikiana na Idara ya Dawa ya Chelsea nchini Uingereza. Inaelezwa kuwa, uwezo huo unatokana na virutubisho vya iridoids, minecoside na specioside vinavyopatikana katika mazao ya mti huo.Mtafiti mahiri Owolabi na wenzake Omogbai walikariri wakisema kuwa, unga unaotokana na kusagwa matunda au mizizi ya mvunge iliyokauswa, unapochemshwa katika maji hutoa faida sawa na dawa zinazotumika kutibu maambukizi ya bakteria wa aina mbalimbali zinazofahamika kama amoxillin.

Jinsi ya kutumia
Kupata faida hizo kwa kutumia mizizi ya mti huo, chukua mizizi au magome yake na uyakaushe kivulini (sio juani), baada ya kukauka, saga magome hayo ili upate unga.
Chota unga huo kiasi cha gramu 700 (karibu na robo tatu kilo), changanya na maji kiasi cha lita kiasi cha lita 6. Mwenye tatizo anatakiwa kunywa mchanganyiko huo kwa kiasi cha robo lita kila siku.

Huongeza ukubwa wa matiti
Ripoti ya Kisayansi ya mtaalamu wa tiba kwa kutumia mimea na vitu vya asili (pharmacognosist ), Simon Jackson pamoja na mtaalamu wa masuala ya mazingira na viumbe hai Bi. Katie Beckett, iliyochapishwa katika jarida linalofahamika kwa jina la Jounal of American Botanical Council, ilieleza kuwa, huko nchini Cape Verde, hutumia matunda ya mti huo kuongeza ukubwa wa matiti. 

Jinsi ya kutumia
Ripoti hiyo iliongeza kueleza kuwa, wasichana wa nchi hiyo hutumia matunda hayo kuongeza matiti, ambapo huchukua matunda hayo na kuyakata kasha husugua katika katiti.

Huongeza urefu wa uume, makalio na hips
Ripoti hiyo ilienda mbali zaidi na kueleza kuwa, huko nchini Afrika Kusini katika jimbo la Limpopo hutumia matunda hayo kuongeza ukubwa wa maumbile ya nyeti za wanaume.
Pia huko nchini Zimbabwa nako watu wa kabila la shona huutumia mti huo katika kuongeza ukubwa wa maumbile ya kiume, lakini huamini dawa hiyo hufanya kazi zaidi inapotumiwa kwa vijana wawadogo kuliko watu wazima.

Aidha, mwanzoni mwa mwaka 2013, gazeti moja la hapa nchini lilimkariri Kaimu Msajili wa Tiba Asili na Tiba Mbadala nchini, Dk. Naomi Mpemba akitoa maelezo yanayo thibitisha juu ya
uwezo wa mti wa Mvunge katika kuongeza urefu wa nyeti za mwanaume, pamoja na matiti na makalio kwa upande wa kina mama.

Jinsi ya kutumia
Inaeleza kuwa, utomvu wa tunda hilo hutumika katika kuongeza maumbile hayo, ambapo muhusika anatakiwa kuchanja katika eneo husika na kupaka utomvu huo.
Njia nyingine ni ile ya kutumia unga unga unaotokana na mti huo, ambapo unga huo huchemsha na kisha muhusika kutakiwa kunywa mchanganyiko huo. Inaelezwa pia, vijana wa kiume nchini Zimbabwe huchimba mizizi ya mvunge na kuitafuta ili kuongeza maumbile ya nyeti zao.

Hutibu vidonda
Ripoti ya Simon Jackson pamoja na Bi. Katie Beckett, iliyochapishwa katika jarida linalofahamika kwa jina la Jounal of American Botanical Council, ilieleza kuwa, unga unaotokana na matunda ya mti huo yaliyokaushwa au magome, hutumika kutibu vidonda au majareha mwilini.
Inaelezwa kuwa, uwezo huo unatokana na msombo (compound) unaofahamika kwa jina la β-sitosterol, unaopatikana katika mazao ya mti huo.

Jinsi ya kutumia
Ripoti hiyo, ilieleza kuwa, unga huo hunyunyuziwa katika nguo au kitambaa na kisha nguo au kitambaa hicho hufungwa katika kidonda au jereha na baada ya siku kadhaa jeraha hilo hukauka.

Hutibu matatizo ya tumbo, minyoo kwa watoto
Ikiendelea kufafanua ripoti hiyo ilisema, magome ya mti huo hutumika kutibu matatizo ya tumbo kwa watoto ikiwemo minyoo. Pia magome hayo, hutibu ugonjwa wa nimonia (pneumonia).

Jinsi ya kutumia
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, kupata tiba ya nimonia na matatizo ya tumbo ikiwa ni pamoja na minyoo kwa watoto, magome ya mvunge huchukuliwa na kulowekwa kwenye maji kisha mtoto mwenye tatizo la tumbo hunywesha maji hayo. Aidha, unaweza kutumia mizizi kama mbadala wa magome kutibu nimonia (pneumonia).

Hutibu muwasho, kutoka ucchafu ukeni, kuvurugika kwa mzunguko wa hedhi
Kwa mujibu wa ripoti ya utafiti uliofanywa na wanasayansi kutoka Idara ya Kemia ya Chuo Kikuu cha Ilorin, nchini Nigeria wakishirikiana na wanasayansi kutoka Idara ya Saynsi ya Kemikali ya Chuo Kikuu Teknolojia cha Bell ulibaini kuwa mazao ya mti huo yana uwezo wa kutibu matatizo katika via vya uzazi vya mwanamke.

Ripoti ya utafiti huo, iliyochapishwa katika jarida linalofahamika kwa jina la African Journal of Pure and Applied Chemistry (Vol. 3 September, 2009) ilieleza kuwa, mizizi na maua ya mti huo ndiyo yanayotumika kupata tiba ya matatizo ya via vya uzazi vya mwanamke.
Matatizo ya via vya uzazi vya mwanamke yaliyotajwa katika ripoti hiyo ni pamoja na muwasho ukeni, kutokwa na uchafu ukeni, na kuvurugika wa mpangilio wa hedhi.

Jinsi ya kutumia
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, mizizi au maua ya mti huo, huchemshwa au kukaushwa na kusagwa kisha huchanganywa na maji, kupata dawa ya matatizo hayo. Baada ya kupata dawa hiyo, muhusika anaweza kuitumia kwa kunywa kwa kipimo cha robo lita na nyingine kujisafishia sehemu za siri.

Hutibu malaria
Nao utafiti uliofanywa na Chuo Kikuu cha California- Berkeley ulibaini kuwa msombo (compound) wa naphthoquinones unaopatikana katika mizizi ya mti huo, una uwezo mkubwa wa kupambana na vimelea vya ugonjwa huo vinavyfahamika kama Plasmodium falciparum.

Jinsi ya kutumia
Kupata tiba ya malaria, magome na majani ya mti wa mvunge huchemshwa kwenye maji kisha mgonjwa hutaiwa kunywa maji hayo kwa kipimo cha robo lita.

Faida zingine
Kwa mujibu wa ripoti ya Jackson na Bi Katie, utafiti uliofanywa na Chuo Kikuu cha Illinois, kilichopo Chicago, ulibaini kuwa huko nchini Malawi hutumia mizizi na matunda ya mti huo kutibu saratani ya mji wa mimba (uterus cancer). Aidha utafiti uliofanywa na Houghton mwaka 1994, ulibaini kuwa magome ya mti huo yanauwezo wa kutibu saratani ya ngozi.Kwa mujibu wa ripoti ya Jackson na Bi Katie, mbegu za mvunge huchomwa na kuliwa, ambapo zinaelezwa kuwa chanzo kizuri cha nishati ya mwili, madini ya phosphorous, protein na mafuta. Mbegu hizo pia hutoa mafuta yenye utajiri wa virutubisho vya oleic acid na fatty acids.

Sambamba na hayo, ripoti hiyo iliongeza kueleza kuwa, majani ya mvunge yaliokaushwa yana virutubisho vya amino acids, madini ya calcium, magnesium pamoja na madini chuma.
Ripoti hiyo iliongeza kuwa, mizizi na magome ya mti huo yana misombo (compounds) za naphthoquinone lapachol na dihydroiso coumarin. Misombo mingine inayopatikana katika magome ni naphthaquinoids kigelinone, pinnatal, isopinnatal, sterols stigmasterol na beta-sitosterol.
Matunda yana misombo ya flavonoids na luteolin. Virutubisho vingine vinavyopatikana katika mazao ya mti huo ni iridoids, saponins na tannins. Matunda ya mti huo yaliyoiva ama mabichi huwa hayaliwi kwani yanaelezwa kuwa na sumu. Ingawa kwa baadhi ya nchi kama vile Kenya hutumia matunda hayokuterngenezea pombe.

7 comments:

  1. Ahsante doctor je kama nina mimba changa na nataka kutumia hiyo dawa je ina madhara kwa mtoto aliyeanza kutungwa tumboni?

    ReplyDelete
  2. Kutana na mtaalamu wa mitishamba anatibu ugumba uzazi.. nguvu za kiume .. kukuza uume kwa mvunge..kuku ku shape hips na makalio ..kupata watoto Pacha .. mpigie Dr kupitia 0744903557 tanga

    ReplyDelete
  3. Kwa tatizo la vidonda vya tumbo je inaweza kutibu tatizo hilo

    ReplyDelete
  4. *MAAJABU* *YA* *MAFUTA* *ASILI* *YA* *MTI* *WA* *MNYONYO* *(CASTOR OIL ). Ni Mafuta Ya Asili *_yaliyoshika umaarufu mkubwa Duniani kutokana na nguvu yake kubwa inayofanya kazi katika mwili wa mwanadamu kuliko mafuta mengne yoyote Duniani!! Mafuta ya Asili ya mti wa Mnyonyo (CASTOROIL) hufanya yafuatayo katika mwili::;
    1: Hutibu fangasi sugu wa aina zote kwa siku tatu
    2: Huondoa makovu na michirizi ndani ya wiki mbili
    3: Hukuza nywele, kusafisha kichwa, kuondoa MBA sugu na kurejesha Afya ya Nywele
    4: Huondoa kipara kwa kujaza nywele na kuzirefusha ndani ya mwezi mmoja
    5: Hutibu U.T.I sugu pamoja na kuondoa gesi tumboni kwa mda cku nne
    6: Husaidia katika kupanga uzazi kwa akina mama bila kutumia njia za kisasa ambazo nyingi zina madhara
    7: Hutibu saratani ya ngozi pamoja na mkanda wa jeshi
    8: Hutibu matatzo yote ya ngozi
    9: Hutibu matatizo ya hedhi kwa akina dada na akina mama
    10: Huondoa mikunjo ya ya ngozi usoni inayomfanya mtu kuonekana mzee,na badala yake huifanya ngozi kuwa nyororo na ya kuvutia
    11: Ni mafuta mazuri kwa watoto wachanga kwa sababu yana Antibiotic-Asili ya kuua vimelea vya magonjwa
    12: Hutibu vidonda vya kuungua kwa moto na aina zote za vidonda sugu katika mwili
    13: Hutibu tatizo la (joint fluid) kuuma kwa joint za mwili kwa kujaa maji pamoja na maumivu
    14: Hutibu kuteguka kwa Mifupa,kuuma kwa baadhi ya sehemu za mwili pamoja na vichomi vya aina zote!!!

    NB!! Mafuta Asili ya mnyonyo(Castor oil) ni yale ambayo hayajapita kiwandani wala kuongezewa kemikali yoyote,tumia yaliyoandaliwa kwa njia za asili zaidi na tatizo lako litakwisha!!!

    NB:: Matumiz ya mafuta haya ni mengi na ni zaid ya yaliyotajwa hapo juu!! Kwa Sababu Dunia yetu hii ni kama kijiji kimoja, mambo yote yapo mtandaoni!! Ingia Google andika" MAFUTA YA MNYONYO" utaona kila kitu!! Kwa uhitaj wa Mafuta haya unaweza kututafta kwa 0621399120 au 0763105115 TUPO CHUO CHA MIPANGO DODOMA!!

    ReplyDelete
  5. Dr Mimi nataka dawa ya kuongeza uume na nguvu

    ReplyDelete
  6. Na Niko Kenya nitapataje?

    ReplyDelete
  7. "Niligunduliwa na saratani ya hatua ya 4 na nikapewa miezi ya kuishi. Kwa kukata tamaa, niligeuka kwa Dk. Dawn, ambaye mpango wake wa matibabu wa ubunifu na usaidizi usio na shaka ulibadilisha kila kitu. Ndani ya wiki, nilihisi kuwa na nguvu zaidi, na baada ya miezi ya huduma yake, uchunguzi wangu haukuonyesha athari ya kansa. Utaalamu na huruma ya Dk. Dawn ilinipa maisha yangu nyuma-nina uthibitisho hai wa kazi yake ya muujiza!"
    Ninapendekeza Dr Dawn kwa mtu yeyote anayepambana na saratani, UKIMWI, herpes na kadhalika, tuma barua pepe, dawnacuna314@gmail.com
    Whatsapp: +2349046229159

    ReplyDelete